November 22, 2013





Nyota wa Yanga, Jerry Tegete na Said Bahanuzi, wanatarajiwa kukiongoza kikosi cha vijana cha timu hiyo ‘U-20’, kitakachoshuka dimbani kesho kuchuana na Saigon, katika mchezo wa fainali Kombe la Etihad ‘Street Soccer Cup’.


Katika mchezo huo, utakaopigwa kwenye Uwanja wa Mwananyamala, Yanga walitinga hatua hiyo baada ya kuwabamiza Faru FC kwa mabao 6-2 huku Saigon wakifuzu kwa kuwachapa Makumbusho Talents kwa mabao 4-3.

Wakati Tegete na Bahanuzi wakiongoza safu ya Yanga, Saigon wanajivunia uwepo wa straika wa Mtibwa Sugar, Mohamed Mkopi, ambaye alifunga mabao yote ya Siagon dhidi ya Talents.

Akithibitisha uwepo wa nyota hao, mratibu wa michuano hiyo Saleh Dunga alisema: “Tayari wamethibitisha hilo, wamekuja baada ya kuona wachezaji wengi wapo kwenye Michuano ya Uhai, inayoendelea jijini Dar,” alisema Dunga na kuongeza kuwa pia kutakuwa na nyota wengine wa ligi kuu.

Bingwa ataondoka na kiasi cha Sh milioni 2 na kombe, wa pili atapata Sh milioni moja na watatu akiweka kibindoni laki tano.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic