Kampuni ya mawasiliano ya
Airtel imemtangaza Rashid Kagomola, mkazi wa Bukoba mkoani Kagera kama mshindi
wa tiketi mbili na safari iliyolipiwa ya kwenda kuangalia moja kwa moja (live)
mechi ya Ligi Kuu ya Uingereza katika uwanja wa Old Trafford.
Kagomola alishinda safari
hiyo wakati wa droo ya kila wiki ya promosheni ya ‘Mimi Ni Bingwa’ inayolenga
kuwazawadia wateja waaminifu, iliyoingia katika wiki ya pili.
Anakuwa mshindi wa pili
wa tiketi baada ya Dickson Lyatuu kutoka mkoani Arusha, kuibuka mshindi wa
kwanza.
Akitangaza mshindi wa
tiketi hiyo katika wiki ya pili, washindi wawili wa shilingi milioni 5 na
washindi wanne wa shilingi milioni moja kila mmoja, Meneja Uhusiano wa Airtel
Tanzania, Jackson Mmbando alisema washindi wote wa tiketi watapewa nafasi ya
kuchagua mtu mmoja watakaesafiri nae kwenda Uingereza, kuangalia mechi ya
Manchester United katika uwanja wa Old Trafford.
“Tunafuraha kutangaza
kuwa mshindi wetu wa tiketi ya kweneda Old Trafford wa droo yetu ya pili ya
promosheni ya ‘Mimi Ni Bingwa’ kuwa ni Rashid Jacob Kagomola atakaeungana na
Bw. Dickson Lyatuu aliyeshinda tiketi ya kwanza na wengine 11 watakaojishindia
tiketi baadae kwenda kuangalia mechi moja kwa moja (live) katika uwanja wa Old
Trafford katika mwezi huu wa kwanza wa droo yetu.
“Kagomola alichaguliwa
baada ya namba ya mtu wa kwanza kujitokeza, kushindwa kupokea simu baada ya
kumpigia mara tatu. Kwa maana hiyo napenda kumuasa kila aliyejisajili katika
droo hii kujiweka tayari kupokea simu kutoka Airtel kwa sababu anaweza kuibuka mshindi,”
alisema Mmbando.
Aliwataja Godfrey David
Msiu kutoka Arusha na Junior Ashery Pesambili, mkazi wa Arusha mjini kuwa
washindi wa shilingi milioni tano kila mmoja wa wiki hii na wateja wengine
wanne waliojishindia shilingi milioni moja kila mmoja.
Mmbando alisema kuwa bado
zawadi nyingi zaidi kushindaniwa na kuongeza kuwa ili kushiriki katika
promosheni hiyo mteja anatakiwa kutuma ujumbe mfupi (SMS) ukiwa na neon
“BINGWA’ kwenda namba 15656.
Alisema kuwa Airtel pia
imeweka vituo maalum kwa ajili ya wapenzi wa Man U kuangalia mechi za
Manchester United bure kupitia luninga kubwa, na kuyataja maeneo hayo kuwa,
Mbeya – Shaba Pub, Mwanza – Shooters Pub, Dodoma – Four Ways, Dar es Salaam –
Rose Garden, Morogoro – Nyumbani Lounge na mkoani Arusha ni Empire Sports Bar.
Droo hiyo ilishuhudiwa na
wawakilishi kutoka katika Bodi ya Michezo ya Kubahatisha ya Tanzania.
0 COMMENTS:
Post a Comment