December 23, 2013


Kiungo mshambuliaji wa Simba, Uhuru Selemani, juzi alijikuta akimpiga ngumi shabiki wa Yanga, baada ya kuambiwa maneno machafu katika mchezo baina ya timu hizo kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.


Tukio hilo lilitokea nje ya uwanja ambapo Uhuru alikuwa akienda kumsalimia mshambuliaji wa Yanga, Emmanel Okwi aliyekuwa na shabiki huyo, ndipo alipokutana na lugha chafu.

Shabiki huyo aliyekuwa kavua jezi huku mgongoni kajiandika ‘Ngassa+Okwi Sawasawa na Kifo’, hakufurahishwa na kitendo cha Uhuru kusalimiana na Okwi ambaye alikuwa akiongea naye, ndipo akamwambia: ‘Nyie Simba wachawi’, kitendo kilichomuudhi nyota huyo wa Simba aliyekuwa amembeba mtoto wake ambapo alimuweka chini na kumrushia ngumi kali.

Baada ya timbwili hilo kutokea, Okwi alimuomba Uhuru atulie, aachane na shabiki huyo ndipo Uhuru aliaga na kuondoka kwa hasira eneo hilo.  


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic