Mwenyekiti aliyesimamishwa wa Simba,
Ismail Rage, amefanya kikao na baadhi ya wanachama wa timu hiyo na kutoa siri
kwamba waliomuuza mshambuliaji Emmanuel Okwi kwa Yanga ni Waganda, SC Villa
lakini akasisitiza ni hujuma kutoka ndani ya klabu hiyo.
SALEHJEMBE ilikuwa ikipata
‘live’ kila kinachoendelea ndani ya kikao hicho kilichofanyika makao makuu ya
klabu ya Simba, barabara ya Msimbazi jijini Dar es Salaam, jana.
Akionyesha mwenye masikitiko, Rage alisema
kuna baadhi ya viongozi wa klabu hiyo wanahusika katika usajili wa Okwi aliyetua
Yanga kwa mkataba wa miaka miwili na nusu.
Rage, amesema Okwi raia wa Uganda, mpaka
sasa anakabiliwa na kesi tatu muhimu na kuzitaja ya kwanza ni ile ya nyota huyo
kukakabiliwa na mashtaka ya kutoroka katika klabu yake ya zamani ya Etoile du
Sahel ya Tunisia (ESS).
Shitaka la pili ni kuhusu SC Villa,
ambao walipewa Okwi kwa mkopo lakini wakamuuza Yanga na tatu ni kesi yake
aliyoifungua Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) kuhusu ESS, ambapo kabla ya
shirikisho hilo kutoa majibu nyota huyo kukubali, Mganda huyo kauzwa Yanga.
“Nilipiga simu Fifa kutaka kujua kujua
kuhusu Okwi, nikaambiwa kuna fedha dola 5,900 ambazo ni kwa ajili ya
kusikilizwa kwa kesi yetu, mwisho ilikuwa saa nne asubuhi leo (jana). Barua
ilishatumwa tangu Desemba 6, lakini hakuna aliyeijibu na wakaificha,” alisema
Rage akitaka kudondosha chozi ‘live’.
“Saa tatu asubuhi nikatuma fedha hizo
ambazo zitatoa nafasi ya kusikilizwa kwa jambo hilo. Kama ningechelewa, basi
Okwi angeweza kuwa mchezaji huru kwenda Yanga,” alisema Rage katika kikao hicho
kilichofanyika kuanzia saa 10:15 hadi saa 11:45 jioni.
Aidha, Rage amesema anajua kuwa kamati
ya utendaji ya timu hiyo inachangia kumhujumu ili aonekane hafai katika klabu
hiyo, ambapo sasa ataitisha mkutano mkuu Januari mwakani.
“Simba imejaa wanafiki, wanafanya mpango
wachezaji waende Yanga. Mfano, Okwi alishatangaza anaitaka Simba, vipi
hawakumsajili na utaona mambo yanaharibika kila nikiwa nje ya nchi. Pia TFF
kuna watu kama hao na wanachangia kutuhujumu na kuniharibia,” alisema.
Kuhusiana na suala la uchaguzi, Rage
rasmi ametangaza kwamba hatagombea nafasi hiyo tena na badala yake kuna mtu
amemuandaa.
“Tayari nimemuandaa mtu, siwezi kumtaja
sasa ila nitawaacha wanachama waamue utakapofika uchaguzi,” alisema Rage.
Mzigo wa Okwi umekuwa ukimuangukia Rage kwa kuwa ndiye alifunga safari
kwenda kumuuza Tunisia, lakini akarejea mikono mitupu na dola
sasa kama anawajua anachosubiri nini hasa pale simba, si ajiuzulu tu na kuwaachia nafasi hao wanaomhujumu na yy abaki kuwa mwanachama tu wa simba.?
ReplyDelete