December 25, 2013





Mshambuliaji wa Yanga, Emmanuel Okwi, raia wa Uganda ametimka nchini na kurudi kwao Uganda kufuatia matatizo ya kifamilia yanayomkabili.
Okwi alitua Yanga wiki iliyopita ambapo alicheza mechi ya ‘Nani Mtaani Jembe’ dhidi ya Simba, mchezo ambao timu yake ilichapwa mabao 3-1.


 Kocha Msaidizi wa Yanga, Fred Minziro, alisema Okwi aliondoka mara baada ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Simba na kudai kuwa atarudi mara baada ya Krismasi.
“Okwi ameondoka nchini amerudi kwao kufuatia matatizo ya kifamilia na atarudi baada ya Krismasi.
“Ameomba ruhusa kwa uongozi na umempa ruhusa hivyo na tunaamini kuwa atakuwa kwenye mazoezi ya timu hii Ijumaa ijayo,” alisema Minziro.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic