Uongozi wa Coastal Union umesema
hautamuongeza mkataba mshambuliaji Haruna Moshi ‘Boban’ kutokana na kuwa na
utovu wa nidhamu.
Alisema kwa tabia ambayo ameionyesha ni
ngumu kumuongeza mkataba mshambuliaji huyo aliyebakiza miezi sita tu katika
mkataba wake unaomalizika mwishoni mwa msimu huu.
Aliongeza pia kutokana na kutojiunga na
kikosi hicho mpaka sasa atakatwa mshahara wake wa mwezi huu kwa kuwa
hajaufanyia kazi yoyote tokea alipotakiwa kujiunga na wenzake Desemba,
Mosi mwaka huu.
Aidha alisema adhabu hiyo itamkuta pia
kiungo Jerry Santo ambaye ni raia wa Kenya kutokana na kutotoa sababu zozote za
kuchelewa kujiunga na wenzake kambini.
“Ni bora tukapandisha vijana wetu wa
U20 kwa kuwa tunajua watatusaidia na wana nidhamu ya hali ya juu kuliko hawa
ambao ni wazoefu lakini wanatusumbua upande huo.
“Hatuwezi kumuongeza mkataba mtu ambaye
tunaona kabisa nidhamu yake haituridhishi kama timu na hajatoa hata taarifa
yoyote. Wa nini mtu kama huyo? Sisi tunaangalia maslahi ya timu ili
ifanye vizuri,” alisema Mnguto.
Boban aliondolewa kwenye kikosi cha
Simba ambacho alikuwa amekitumikia kwa muda mrefu kutokana na utovu wa nidhamu.
0 COMMENTS:
Post a Comment