December 27, 2013




Timu ya Majimaji inatarajia kupiga kambi kuanzia kesho Jumamosi katika mji mdogo wa Peramiho, Ruvuma ili kujiandaa na raundi ya pili katika Ligi Daraja la Kwanza.


Meneja wa timu hiyo Godfrey Mvula amesema safari hii wamejipanga kucheza mechi nyingi za kujipima ubavu nje ya mkoa pia amewataka wadau wa soka kuchangia timu yao kwa moyo mmoja ili kuimarisha timu hiyo ambayo inategemea bakuli toka kwa wanachama.

Kambi hiyo ipo kwenye eneo la Hospitali ya Peramiho ambapo mara kadhaa timu hiyo imewahi kuungwa mkono na madaktari wa hospitali hiyo.

“Tunaingia kambini mwisho wa mwezi huu, wadau na wapenda mpira mkoani Ruvuma wajitokeze kwa wingi kuchangia timu yao kwa kuwa haina fedha na inategemea toka kwao hivyo lazima wajitoe kwa hali na mali,” alisema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic