Mashabiki wa FC Porto ya Ureno wametoa kali ya mwaka baada ya
kulizuia basi la wachezaji wao.
Mashabiki hao walilizuia basi hilo wakionyesha hasira kali baada
ya timu yao kupoteza mechi dhidi ya Academica, walifungwa bao 1-0.
Porto haikuwa imepoteza hata mechi moja katika michezo 53
ilizocheza hadi ilipofungwa na Academica.
Kilichowaudhi mashabiki hao ni kuona timu yao inafungwa na timu
iliyo mkiani, wakasisitiza kwamba waliidharau, ndiyo wamepoteza hivyo walitaka
kuwapa somo.
0 COMMENTS:
Post a Comment