Baada ya mvutano wa hapa na pale,
hatimaye kiungo Selemani Matola ameanza kazi ya kocha msaidizi chini ya Kocha
Zradkov Logarusic.
Awali ilionekana Logarusic kukerwa na
kuchelewa kwa Matola, lakini baadaye kukawa na taarifa kocha huyo wa vijana wa
Simba alikuwa akisubiri ajadili mkataba wake mpya kama kocha msaidizi.
Lakini leo Matola ameungana na
Logarusic na kuanza kupiga job kwenye Uwanja wa Kinesi jijini Dar es Salaam.
Taarifa zimesema tayari Matola
amefanya mazungumzo na uongozi wa Simba chini ya kamati ya utendaji na utampa
mkataba mpya ambao umeboreshwa.
Matola ni kati ya makocha vijana
wenye uwezo mkubwa na amekuwa akipigiwa chepuo kupewa timu kubwa.
Iliwahi kuelezwa angekuwa msaidizi wa
Abdallah Kibadeni, lakini baadaye Jamhuri Kihwelo ‘Julio’, beki wa zamani wa Simba,
akaongezewa miezi sita kuendelea kuinoa timu hiyo.
Kibadeni na Julio wameondolewa Simba
na nafasi zao sasa zitarithiwa na Logarusic raia wa Croatia na Matola ‘raia’ wa
Kigoma.
0 COMMENTS:
Post a Comment