December 27, 2013





Klabu ya Simba ipo kwenye mikakati ya kutafuta nyumba kwa ajili ya kocha wao, Mcroatia Zdravko Logarusic na wachezaji wapya wa timu hiyo.


Ofisa Habari wa Simba, Stanley Philip amesema uongozi kwa sasa unalifuatilia suala hilo kwa kutafuta nyumba ya kisasa kwa ajili ya kocha na wachezaji wapya wa kikosi hicho.

Alisema mchakato huo ulianza mapema lakini hawakupata iliyokidhi viwango hivyo watahakikisha watakaporejea kwenye Michuano ya Mapinduzi atafikia nyumbani kwake.

Upande wa beki wao Mkenya, Donald Musoti, Philip alisema amerejea kwao kuchukua vitu vyake alivyoviacha kisha atarejea leo Ijumaa.

 “Tupo kwenye mchakato wa kutafuta nyumba ya kisasa ya Kocha Loga pamoja na wachezaji wengine wapya waliojiunga nasi haijalishi maeneo gani ilimradi tu nyumba iwe na ubora,” alisema Philip.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic