December 27, 2013





Beki wa kati wa Coastal Union ya Tanga, Juma Nyosso amefurahia kupewa majukumu ya kuwa nahodha wa timu hiyo.
 
Nyosso, beki wa zamani wa Simba alipewa majukumu hayo juzi Jumatano baada ya kocha mkuu wa timu hiyo, Yusuph Chippo kumvua cheo hicho nahodha wa awali wa timu hiyo, Mkenya Jerry Santo aliyechelewa kurejea klabuni kutoka kwenye mapumziko.

Nyosso amesema kuwa amefurahishwa na unahodha huo kwa kuwa ni kitu kizuri kwa mchezaji kuaminiwa na kupewa wadhifa kama huo kwenye klabu kubwa kama hiyo nchini.

“Nimefarijika kwa kweli na ni kitu kizuri kwangu japo naona kama ni kawaida kwa kuwa nilishawahi kuwa nahodha huko nyuma, lakini kutokana na ukubwa wa timu ni kitu cha faraja sana kwangu,” alisema Nyosso.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic