Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),
limeweka wazi kuwa halitamuongezea ajira kocha wa timu za vijana, Jacob
Michelsen raia wa Denmark.
Uamuzi huo, umetangazwa leo na Rais wa
TFF, Jamal Malinzi, ambapo amesema shirikisho lake limeona hakuna sababu ya
kumuongezea mkataba kocha huyo, ambao
unamalizika 15 Desemba, mwaka huu.
Malinzi, amesema mara baada ya mkataba huo wa Michelsen kumalizika, TFF
itamsaka mrithi wake, ambapo sasa Mtanzania atachukua nafasi ya Mdenish huyo,
ukiwa ni mkakati maalum wa kuwapa wazawa nafasi.
“Tumeona hakuna haja ya kumuongezea
mkataba Jacob (Michelsen), mkataba wake wa sasa unafikia tamati Desemba 15,
mwaka huu na utakapomalizika ataondoka mara moja na tayari tumeshamjulisha
mapema juu ya uamuzi huo,” alisema Malinzi.
“Tumekubaliana kama TFF, kwamba mara
baada ya Jacob kuondoka nafasi yake atafutwe kocha wa Kitanzania, mwenye uwezo
ili azibe nafasi yake, hii ni katika kuwapa nafasi wazawa wenye uwezo wa
kufanya majukumu haya, tunajua kuwa watu makini wapo.
0 COMMENTS:
Post a Comment