Klabu ya Yanga imetangaza kupata hasara
ya shilingi milioni 99,454,424 katika mapato na matumizi ya kuiendelesha timu
hiyo inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Katibu
Mkuu wa timu hiyo, Lawrence Mwalusako alisema, hasara hiyo ni kuanzia Januari
15 hadi Aprili 15, mwaka huu.
Mwalusako alisema, jumla ya mapato
yaliyopatikana ni shilingi milioni
293,575,561.35 huku matumizi yakiwa ni 320,034,985.72 ambayo ni mengi
hayaendani na mapato yao.
“Kwa matumizi na mapato hayo tuliyoyatangaza,
tunahitaji kupunguza kupunguza matumizi ya klabu ili kuiendesha klabu yetu kwa
kutafuta vyanzo vya mapato.
“Sehemu ya matumizi inayosababisha
kutumia fedha nyingi ni mishahara ya wachezaji na fedha za kusajilia wachezaji,
hivyo tunahitaji kuuza baadhi ya miradi yetu ikiwemo jezi, skafu na bendera,”
alisema Mwalusako.
0 COMMENTS:
Post a Comment