KIJUSO, WAKATI AKIWA SIMBA |
Mshambuliaji wa Mbeya City, Mohamed
Said Kijuso amekabidhiwa king’amuzi na wadhamini wa Kombe la Mapinduzi kutokana
na kuwa mchezaji wa kwanza kufunga bao kwenye Uwanja wa Gombani, juzi.
Mbeya City ilipata sare ya 1-1 dhidi
ya Clove Stars, hivyo wadhamini wa michuano hiyo, Azam TV wakamzawadia straika
huyo mkongwe ambaye alifunga katika dakika ya 14 King’amuzi hicho.
Kijuso ameliambia gazeti hili kuwa
amejisikia furaha kubwa japokuwa timu yake haikushinda mechi hiyo.
“Nimefarijika sana kuweza kuipatia timu yangu bao pekee katika mchezo huo.
Mechi ilikuwa nzuri lakini jamaa walitukamia sana,” alisema Kijuso.
0 COMMENTS:
Post a Comment