January 3, 2014




Na Abdi Suleiman, Zanzibar
Simba juzi ilifanikiwa kuanza vizuri Michuano ya Kombe la Mapinduzi kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya AFC Leopard ya Kenya, huku viungo wa timu hiyo, Ramadhan Singano ‘Messi’ na Haruna Chanongo wakionyesha uwezo wa juu.


Katika mechi hiyo iliyochezwa juzi usiku kwenye Uwanja wa Amani Mjini Unguja, huku Mgeni rasmi akiwa ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, Simba ilipata bao katika dakika ya 77 mfungaji akiwa ni Amir Kiemba, aliyeunganisha krosi ya Messi.

Wakati huohuo, Kocha Mkuu wa Mbeya City, Juma Mwambusi amewataka waamuzi wanaochezesha michuano hiyo kufuata sheria 17 za soka wanapokuwa uwanjani, kauli ambayo ameitoa baada ya timu yake kupata sare ya bao 1-1 dhidi ya Clove Ster, juzi kwenye Uwanja wa Gombani, Pemba.

“Mchezo ulikuwa mzuri muda wote, ila maamuzi ya refa yalikuwa yakitukera,” alisema Mwambusi. Matokeo mengine ya michuano hiyo kwa mechi za juzi, KMKM ilifungwa 3-2 na KCC ya Uganda.
SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic