Shrikisho
la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limeteua Watanzania Alfred Rwiza Kishongole na
Lina Kessy kuwa makamishna wa mechi za shirikisho hilo zitakazochezwa wikiendi
ya Februari 14 mwaka huu.
Kishongole
ameteuliwa kusimamia mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Cote d’Or ya
Shelisheli na Kabuscorp de Palanca ya Angola.
Mechi hiyo
ya marudiano ya raundi ya mchujo itafanyika Shelisheli na itachezeshwa na
waamuzi kutoka Madagascar wakiongozwa na Abdoul Ohabee Kanoso. Waamuzi wengine
ni Basile Alain Rambeloson, Augustin Gabriel Herinirina na Andofetra Avombitana
Rakotojaona.
Naye Kessy
atakuwa kamishna wa mechi ya kwanza ya raundi ya kwanza ya Kombe la Afrika kwa
Wanawake (AWC) kati ya Rwanda na Kenya itakayochezwa jijini Kigali.
Waamuzi wa
mechi hiyo wanatoka Cameroon. Mwamuzi wa kati ni Sylvie Abou wakati wasaidizi
wake ni Winnie li Koudangbe, Lum Rochelle na Jeanne Ekoumou.
0 COMMENTS:
Post a Comment