January 13, 2014


Mshambuliaji wa Mtibwa Sugar, Mussa Hassani Mgosi, amemwambia kinara wa mabao kwenye Ligi Kuu Bara, Amissi Tambwe kwamba akae mkao wa kula kwani anataka kurudisha enzi zake katika mzunguko wa pili.


Mgosi alikuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2009/2010 akiiwezesha Simba kutwaa ubingwa, baada ya kupachika mabao 16.

Ingawa Mgosi hakuifungia Mtibwa bao lolote katika mzunguko wa kwanza kutokana na kutocheza mechi nyingi kufuatia kuwa majeruhi, amesema anataka kurejesha enzi zake katika mzunguko wa pili na suala la kumfikia Tambwe mwenye mabao 10 ni la mechi kadhaa tu. 

Mgosi alisema anaendelea kujipanga vizuri ili atimize lengo lake hilo.

 “Ninajipanga ili nionyeshe maajabu katika mzunguko ujao, nia yangu ni kuhakikisha timu yangu ya Mtibwa inafanya vizuri na kuchukua nafasi nzuri kwenye ligi Kuu, ikiwa ni pamoja na kutupia mabao ya kutosha, hasa nikitazamia kuchukua nafasi ya mfungaji bora kwa mwaka huu.

“Namuomba sana huyo Tambwe ajipange vizuri, maana mimi ni mkongwe na ni mtaalamu wa kutikisa nyavu, hivyo kuongoza kwake mzunguko wa kwanza asibweteke maana nimejipanga kuisaidia timu na ikiwezekana nitahakikisha hadi ligi inamalizika niwe naongoza kwa ufungaji bora,” alisema Mgosi.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic