January 2, 2014



 
LOGARUSIC AKIWA MAZOEZINI NA MENEJA, NICO NYAGAWA. HII ILIKUWA SIKU CHACHE KABLA YA MATOLA KUANZA KAZI.
Kocha mkuu wa Simba, Zdravko Logarusic ameonyesha kufurahishwa na kazi anayoifanya msaidizi wake, Selemani Matola.
 
Logarusic amesema Matola ameonyesha ni kocha ambaye atakuwa bora zaidi hapo baadaye kwa kuwa anakwenda vizuri.
 
MATOLA AKIWA AMEBEBWA NA WACHEZAJI WA SIMBA B BAADA YA KUTWAA KOMBE LA BANC ABC, MWAKA JANA.
“Kabla ya kuondoka tulipanga mambo kadhaa muhimu kuhusiana na mechi dhidi ya AFC na kila kitu amefanya kama ilivyotakiwa,” alisema.

“Nimefurahishwa naye sana, nampongeza na kutaka kuendelea kujituma,” alisema Logarusic ambaye yuko kwao nchini Croatia kwa mapumziko.

Alisema anatarajia kuja nchini ndani ya siku mbili baada ya mapumziko kwisha kuungana na Simba inayoshiriki michuano ya Mapinduzi mjini Zanzibar.

Katika mechi ya kwanza, Simba ilishinda kwa bao 1-0 dhidi ya FC Leopards ya Kenya ambayo msimu uliopita ilishika nafasi ya pili kwenye Ligi Kuu Kenya.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic