January 3, 2014




Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limewataka wanachama wa Klabu ya Simba kuwasilisha malalamiko yao kwa maandishi kwenye shirikisho hilo kwa lengo la kumaliza lawama za wanachama hao zinazosikika mtaani.


Simba imekuwa kwenye mvutano ambapo kuna baadhi ya wanachama wanampinga mwenyekiti wao, Ismail Aden Rage ambapo mara kadhaa wamejaribu kumuondoa madarakani lakini ikashindikana.

Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura amesema hawajapokea malalamiko yaliyofikishwa kwenye shirikisho hilo zaidi ya kusikia mtaani na kuona kwenye vyombo vya habari.

“Wanachama wa Simba wanatakiwa kufikisha malalamiko yao kwanza kwetu kwa maandishi ndiyo waende kutoa taarifa kwa umma ili tujue tunawasaidia vipi.

“Kwa sasa TFF hatutambui malalamiko yao mpaka watakapoamua kuyaleta rasmi ndiyo tutaanza kuyafanyia kazi,” alisema Wambura.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic