January 15, 2014



 
MKONGWE KIEMBA (WA TATU KULIA) AKIWA NA WACHEZAJI MAKINDA WA SIMBA
Kocha Msaidizi wa Simba, Selemani Matola, amesema kiungo wa timu hiyo, Amri Kiemba, anaweza kucheza soka kwa miaka mitano zaidi.


Kiemba amekuwa chachu ya kufanya vizuri kwa Simba kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi, hali iliyolifanya benchi la ufundi la timu hiyo lifikirie kumpa zawadi.
 
Matola amesema anakiamini kiwango cha Kiemba kutokana na jinsi anavyojituma uwanjani na kudai atacheza kwa muda mrefu akiendelea na tabia yake hiyo.
 
“Kiemba ni mchezaji mzuri na mwenye nidhamu, kitu kinachomfanya awe na kiwango kizuri ni kutokana na kufuata sheria za soka pamoja na kujituma uwanjani.

“Kiwango chake bado kipo juu licha ya umri wake kwenda mbele kwa kuwa ana kipaji pamoja na uwezo wa kucheza mpira, ndiyo maana amefanya vizuri Mapinduzi, hivyo ataendelea kucheza kwa muda mrefu hata miaka mitano mbele,” alisema Matola.

Alimalizia kwa kusema kuwa ataendelea kuisaidia Simba kwa muda mrefu mbele kutokana na kujituma.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic