Young
Africans kesho jumatatu saa 8 mchana kwa saa za nchini Uturuki sawa na saa 9
kamili kwa saa za Afrika Mashariki itashuka dimbani kucheza mchezo wake wa
mwisho wa kirafiki dhidi ya timu ya Simurq PIK inayoshiriki Ligi Kuu nchini
Azerbajain katika viwanja vya Side Manavgat.
Kocha
mkuu wa Young Africans mholanzi Hans Van Der Pluijm amesema watautumia mchezo
huo kama sehemu ya mwisho ya maandalizi ya kujianda na Ligi Kuu ambayo
inatarajiwa kuanza mwishoni mwa wiki ijayo ambapo watoto wa jangwani watafugua
dimba dhidi ya Ashanti United uwanja wa Taifa.
Mchezo
wa kesho utakua mgumu pia, kwani timu ya Simurq PIK ina wachezaji wazuri ambao
wanatoka sehemu mbali mbali dunianina ipo katika nafasi ya tano katika msimamo
wa Ligi Kuu nchini kwao, hivyo nadhani kitakua kipimo kizuri cha mwisho kabla
ya kurejea nchini Tanzania
Kuhusu
kikosi chake mara baada ya mazoezi ya asubuhi, Hans amesema anashukuru mungu
maendeleo ya timu ni mazuri, mabadiliko yapo na wachezaji wanaonekana kumuelewa
hivyo anaamini kadri siku zinavyokwenda timu itakua katika kiwango kizuri
zaidi.
"Nimeshashuhudia
michezo miwili mmoja tukishinda 2-0 dhidi ya timu ya Altay SK Lidi Daraja la
pili Uturuki na jana tukitoka sare ya 0-0 dhidi ya timu ya KS Flumartari ya
Ligi Kuu Albania, kwa kweli nawapongeza vijana wanaonyesha kweli wanajua wajibu
wao na kucheza kwa kufuata maelekezo ya walimu" alisema Hans.
Aidha
Hans amesema ni jambo njema timu imecheza jumla ya michezo mitatu, ikishinda
miwili na kutoka sare mchezo mmoja, huku ikifunga mabao 5 na kutokuruhusu nyavu
zake kutikisika hii yote inayonyesha timu imeiva tayari kwa mashindano
yanayotukabili.
Mpaka
sasa hakuna mchezaji majeruhi hata mmoja kufuatia kiungo Hassan Dilunga kupona
malaria na kuungana na wenzake katika mazoezi.
0 COMMENTS:
Post a Comment