January 16, 2014


Baada ya kurejea jijini Dar es Salaam, Simba inaanza mazoezi leo jioni kwenye Uwanja wa Kinesi.


Kocha Msaidizi wa Simba, Selemani Matola amesema wamepanga kuanza mazoezi leo kwenye uwanja huo kujiandaa na mechi ya Mtibwa Sugar.
“Jumamosi (kesho) tutacheza na Mtibwa Sugar mechi ya kirafiki, lakini leo tunaanza mazoezi pale Kinesi,” alisema Matola.
Simba ilikuwa mjini Zanzibar ilikoshiriki michuano ya Kombe la Mapinduzi na kufanikiwa kuingia fainali lakini ikafungwa bao 1-0 na KCC ya Uganda.

Simba inajiandaa na mzunguko wa lala salama wa Ligi Kuu Bara chini ya kocha wake, Zdravko Logarusic.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic