Na Baraka Kizuguto, Antalya
Young Africans imekamlisha ziara ya kambi yake nchini Uturuki bila ya kupoteza mchezo hata mmoja baada ya leo kutoka sare ya mabao 2-2 dhidi ya timu ya Simurq PIK inayoshiriki Ligi Kuu nchini Azerbajain katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliofanyika jioni ya leo katika viwanja vya Side Star Hotel Complex Manavgat jijini Antalya Uturuki.
Young Africans imekamlisha ziara ya kambi yake nchini Uturuki bila ya kupoteza mchezo hata mmoja baada ya leo kutoka sare ya mabao 2-2 dhidi ya timu ya Simurq PIK inayoshiriki Ligi Kuu nchini Azerbajain katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliofanyika jioni ya leo katika viwanja vya Side Star Hotel Complex Manavgat jijini Antalya Uturuki.
Mchezo wa leo dhidi ya Simurq PIK
ulikuwa ni mchezo wa nne kwa Young Africans tangu kuwasili nchini Uturuki
ambapo imeweza kushinda michezo mwili dhidi ya Ankara Sekerspor 3-0, na Altay
SK 2-0 zote za Ligi Daraja la pili nchini Uturuki kabla ya kutoka sare na timu
ya KS Flamurtari ya Ligi Kuu nchini Albania.
Dakika ya 13 ya mchezo mshambuliaji
wa kimataifa kutoka nchini Burundi, Didier Kavumbagu aliipatia Young Africans
bao la kwanza kufuatia pasi nzuri ya mshambulaji Emmanuel Okwi na Didier
kuukwamisha mpira wavuni na kumuacha mlinda mlango wa Simurq PIK Pawel Kapsa
akiduwaa.
Simuriq PIK walifanya shambulizi
kupitia kwa kwa kiungo wao Stephan Polyak lakini golikipa wa Young Africans
Juma Kaseja alikoa hatari hiyo, huku Tagim Novruzov akishindwa kumalizia mpira
uliotoka sentimeta chache langoni.
Dakika ya 30 ya mchezo Young Africans
ilijipatia bao lake la pili kupitia kwa kiungo Mrisho Ngasa ambaye aliwatoka
walinzi wa Simurq kufuatia migongeo mizuri katika Niyonzima, Okwi , Kavumbagu
na kumkuta Ngasa ambaye aliukwamsiha mpira katika nyavu ndogo.
Mpira wa krosi uliopigwa na nahodha
wa Simurq Ruslan Poladov uliwapita walinzi wa Young Africans wakishindwa
kuucheza na kumkuta mlinzi wa kati Anderson Oliveira aliyepanda kusaidia
mashambulizi aliyeipatia timu yake bao la kusawazisha.
Mpaka dakika 45 za kipindi cha kwaza,
Young Africans 2 - 1 Simurq PIK.
Kipindi cha pili kilianza kwa
Young Africans kufanya mabadiliko ambapo Nadir Haroub "Cannavaro"
aliingia kuchukua nafasi ya Kelvin Yondani huku kiungo Hamis Thabit akichukua
nafasi ya kiungo mkabaji Frank Domayo "Chumvi".
Dakika ya 56 ya mchezo Simuriq PIK
walipata bao la pili na la kusawazisha kupitia kwa mshambulaji wao Murad
Sattarli baada ya kazi nzuri iiyofanywa na kiungo wao Stephan Polyak na mpira
huo kuwapita walinzi wa Young Africans na kumkuta mfungaji.
Mara baada ya bao hilo, timu zote
ziliendelea kushambuliana kwa zamu lakini mpaka dakika 90 za mchezo zinamalizika,
Young Africans 2 - 2 Simurq PIK.
Mara baada ya mchezo wa leo kocha
mkuu wa Young Africans mholanzi Hans Van Der Plyum amesema vijana wake
wamecheza vizuri kwa kufuata maelekezo, ana muda wa wiki moja lakini tayari
anaona mabadiliko kiuchezaji na kutegemea kufanya vizuri katika mashidano
yatakayotukabili.
"Timu imecheza vizuri
nawapongeza vijana kwa kujituma, hakuna lisilowezekana katika mpira, wachezaji
wangu sasa hivi wanajiamini na wanajua wanatakiwa wafanye nini kwa wakati
muafaka, ilikua mechi nzuri sana hata kocha wa Simurq PIK amefurahi uwezo
wetu" alisema Hans.
Mara baada ya mechi ya leo timu
itaendelea na mazoezi kesho asubuhi kuendelea kujiweka fit kabla ya kuanza
safari ya kurejea nchini katikati ya wiki hii tayari kwa ajili ya mzunguko wa
Pili wa Ligi Kuu ya Vodacom na mashindano ya kimataifa.
Young
Africans: 1.Juma Kaseja, 2.Juma Abdul,
3.Oscar Joshua, 4.Mbuyu Twite, 5.Kelvin Yondani/Nadir Haroub, 6.Frank
Domayo/Hamis Thabit, 7.Mrisho Ngasa/Saimon Msuva, 8.Haruna Niyonzima, 9.Didier
Kavumbagu, 10.Emmanuel Okwi, 11.David Luhende/Said Bahanuzi
Simurq PIK:
1.Pawel Kapasa, 2. Ruslan Poladov , 3.Dilaver Zrnanovich, 4.Tural Axundov,
5.Anderson De Oliveira, 6.Tagim Novruzov, 7.Nichat Kurbanov/Bashir Jamilu,
8.Patrick Osiako, 9.Salif Ballo, 10.Rashad Ayyubov, 11.Stepahn Polyak
0 COMMENTS:
Post a Comment