March 8, 2014


Na Saleh Ally, Cairo
Mabingwa wa soka Tanzania Bara, Yanga wanaanza safari leo kutoka Cairo kwenda mjini Alexandria.

Wapinzani wao, Al Ahly ambao ni mabingwa wa Afrika walianza safari hiyo jana na tayari wako kwenye mji huo wa Alexandria.

Mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kuwania kufuzu katika hatua ya 16 Bora kati ya timu hizo mbili inapigwa kesho Jumamosi mjini Alexandria.
Yanga wanaondoka leo asubuhi kwenda huko wakiwa na kikosi kizima wakitumia basi maalum.
Kutoka jijini hapa hadi Alexandria ni mwendo wa takribani saa mbili na nusu.

Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van Der Pluijm amesema muda mzuri wa kuondoka ni hiyo saa nne ya asubuhi hii.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic