March 7, 2014

TAMBWE

Mshambuliaji wa Simba, Amissi Tambwe amepigwa faini ya Sh 500,000 kwa kuonyesha ishara ya matusi wakati akishangilia bao lake.

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limesema Tambwe alionyesha alama ya matusi kutumia kidole chake wakati anashangilia.
MGOSI

Tambwe alifanya hivyo baada ya kuifungia Simba bao wakati ilipoivaa Mbeya City mjini Mbeya.

Mechi hiyo ilimalizika kwa sare ya bao 1-1, Tambwe raia wa Burundi akiwa ni shujaa wa Simba.

Hadi sasa Mrundi huyo ana mabao 17 akiwa kileleni kwa upachikaji mabao.

Naye, mshambuliaji wa Mtibwa Sugar, Musa Mgosi amepigwa faini ya sh. 500,000 kwa kosa la kupiga uwanjani kwenye mechi dhidi ya Ashanti United ambapo vilevile atakosa mechi tatu za ligi. Coastal Union imepigwa faini ya sh. 500,000 kwa washabiki wake kumrushia chupa za maji kipa wa Mbeya City.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic