March 9, 2014

NIYONZIMA AKIWA NA WENZAKE, JANA USIKU
Na Saleh Ally, Alexandria
Kiungo nyota wa Yanga, Haruna Niyonzima raia wa Rwanda ni mgonjwa, malaria kali imemshika, hali iliyolazimika Kocha Hans van Der Pluijm amuondoe kwenye kikosi cha leo kitakachoanza dhidi ya Al Ahly.


NIYONZIMA (KULIA) AKIWA NA OKWI NA MSUVA MWENYE MAZOEZI YA MWISHO YA YANGA, JANA USIKU
Haijajulikana kama Pluijm anaweza kumuweka aanzie benchi lakini taarifa zinasema Didier Kavumbagu anaingia kuanza katika nafasi yake na kocha atajua namna ya kuwapanga, huenda Mrisho Ngassa akacheza namba nane au vinginevyo.


Lakini jana usiku, Niyonzima alikuwa kati ya wachezaji waliofanya mazoezi na wenzake kwenye Uwanja wa Max jijini hapa, lakini leo akaamua malaria ikiwa imemkamata.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic