March 6, 2014

 Na Mwandishi Wetu, Dohar
Kiungo nyota wa Al Markhiya ya Qatar, Mwinyi Kazimoto amesema alitamani kuichezea Taifa Stars katika mechi ya kirafiki dhidi ya Namibia.

Lakini alishindwa kutimiza nia yake hiyo kwa kuwa suala la mawasiliano kati ya TFF na shirikisho la Qatar kuchelewa.
“Imeshindikana, lakini kama nilivyosema awali niliwaombea wafike salama Namibia na kucheza vizuri,” alisema.

“Lakini nilitamani sana kuichezea timu yangu ya taifa katika mechi hiyo. Ninaamini nafasi itapatikana tena,” alisema Kazimoto ambaye sasa ni tegemeo wa kikosi hicho cha Al Markhiya.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic