March 6, 2014


Na Mwandishi Wetu, Windhoek
Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inatarajia kurejea nchini kesho (Machi 7 mwaka huu) kutoka Windhoek, Namibia kwenye mechi ya kirafiki ya kalenda ya Fifa.


Taifa Stars ambayo katika mechi hiyo dhidi ya Namibia (Brave Warriors) ilitoka sare ya bao 1-1 itatua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 12:45 jioni kwa ndege ya South Africa Airways.


Timu inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager baada ya kuwasili itakwenda hoteli ya Accomondia na baadaye taratibu zitafanyika kuvunja rasmi kambi yake.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic