March 7, 2014


Na Saleh Ally, Cairo
KOCHA Mkuu wa Yanga, Hans van Der Pluijm amewataka waandishi wa habari nchin hapa kuwaacha kwa muda wamalizie maandalizi yao.

Pluijm raia wa Uholanzi amewaambia mashabiki hao kwamba wanataka kupiga soka, hivyo hawatakuwa na muda wa mazungumzo kwanza.

“Kazi yangu ni kufundisha soka, kama kuna tatizo la uwanja au vipi, mimi sijui. Sitaki kuzungumza sana, kifupi tuacheni kwanza.
“Kuna maandalizi tunafanya kwa ajili ya kucheza mechi ya Jumapili. Hivyo tuacheni kwanza,” alisema Pluijm alipozungumza na waandishi kwa takribani dakika 10.
Baada ya hapo aliongonzana na Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga, wakaingia kwenye basi lililobeba wachezaji na kuondoka zao.

Yanga imejichimbia mafichoni katika kambi maalum baada ya kuikataa hoteli ya nyota tano waliyopewa na wenyeji wao Al Ahly.
SOURCE: CHAMPIONI NEWSPAPER

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic