March 13, 2014


Kocha wa Yanga, Hans van der Pluijm, amewataka vijana wake kuthibitisha ubora wao katika mechi za Ligi Kuu Bara.

Pluijm amesema anaamini mechi dhidi ya Mtibwa Sugar wikiendi hii itakuwa ngumu kwao lakini lazima waonyeshe kuwa wao ni bora kwa kufanya vizuri.
"Ubora wetu umekuwa juu, kila mmoja kaona katika mechi zetu mbili dhidi ya Al Ahly.
"Lakini lazima tushinde katika mechi za ligi zinazofuata ili kutubitisha kuwa tuna kikosi bora," alisema.
Yanga iling[olewa kwenye Ligi ya Mabingwa na Al Ahly ya Misri baada ya kushinda jijini Dar kwa bao 1-0, halafu ikapoteza kwa idadi hiyo jijini Alexandria.
Ilipoamuliwa mikwaju ya penalti, ikalala kwa 4-3 na kupoteza nafasi ya kucheza 16 bora.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic