March 13, 2014



Kocha wa Simba, Zdravko Logarusic amesema suala la kujituma katika kikosi chake halitakuwa na mjadala.

Logarusi amesema hata kama hawafurahishi baadhi ya watu, lakini atashikilia msimamo wake kuwa lazima watu wajitume.
“Kama kuna mtu atakuwa anagombana nami kwa kuwa tu nataka afanye kazi vizuri na ajitume, wala sitakuwa na hofu.

“Nitashikilia hilo, nitasisitiza lazima afanye kazi kwa juhudi zaidi na halitakuwa ombi, huo ni wajibu,” alisema akionyesha kujiamini.

Loga amekuwa akilaumiwa kwamba hana lugha nzuri kwa wachezaji, lakini wengine wamekuwa wakimuunga mkono kuwa amekuwa akisisitiza wachezaji kujituma.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic