March 13, 2014


Kiungo nyota wa zamani wa Eric Cantona anashikiliwa na polisi wa jiji la London kwa tuhuma za kumdunda mtu.



Taarifa zinaeleza Cantona alitandika mtu ambaye hakutajwa baada ya kupishana kauli wakati wakipata 'kilaji' katika baa moja katika viunga vya jiji la London.

Hata hivyo mitandao mbalimbali ya Uingereza imekuwa ikipishana kuhusiana na suala hilo, mingine imeeleza walitoleana maneno na mitandao mingine inaeleza Cantona alimdunda mtu huyo.
Hata hivyo, taarifa zinasema mtu huyo hakutaka kwenda hospitali badala yake akaamua kufungua mashitaka.


Cantona anajulikana kwa vurugu na maarufu zaidi kupitia lile teke lake la kung fu alilomrukia shabiki mwaka 1995.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic