March 13, 2014

ULI (WA KWANZA KULIA), AKISHEREKEA BAADHI YA MAFANIKIO YA BAYERN

Rais wa Bayern Munich, Uli Hoeness amehukumiwa kwenda jela miaka mitatu na nusu.

Uli amepatikana na hatia kukwepa kodi ya mamilioni ya euro kupitia benki moja nchini Uswiss.
ULI AKIWA NA MKEWE WAKATI AKIWASILI MAHAKAMANI, LEO

Uli mwenye miaka 62 ni mmoja wa watu maarufu nchini Ujerumani, pia katika soka duniani.
Alipatikana na hatia baada ya kukwepa kodi ya pauni milioni 3.5 kupitia akaunti hiyo kwenye benki ya Uswiss.
Lakini baadaye ikagundulika kwamba kulikuwa na ulaghai mwingine wa euro milioni 15.
Hadi anafungwa, Uli alikuwa kiongozi mwenye mafanikio zaidi kwa upande wa klabu kwa kuwa Bayern imekuwa ndiyo timu bora zaidi kwa kipindi hiki.




0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic