Aliyewahi kuwa
Mwenyekiti wa Simba, Hassan Dalali anayeaminika kuwa kiongozi anayependwa zaidi
na wanachama wa klabu hiyo katika kipindi hiki, leo alikutana na Mwenyekiti wa
sasa, Ismail Aden Rage na kupiga stori sana.
Rage
aliomba kupiga picga na Dalali na kusema alichangia yeye kuingia kugombea
uenyekiti wa Simba, lakini leo alitangaza kwa mara nyingine kwamba hatogombea
tena nafasi hiyo katika uchaguzi wa Mei 4, mwaka huu.
RAGE AKIWA NA DALALI |
RAGE AKIKUMBATIANA NA KABURU |
Viongozi hao wamekutana leo kwenye mkutano wa marekebisho ya katiba ya Simba uliofanyika kwenye Ukumbi wa Maofisa wa Pilisi Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Pamoja na
hivyo, Rage alikumbatiana na aliyekuwa makamu mwenyekiti wakati wa uongozi
wake, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ ambaye ilielezwa wamekuwa wapinzani kwa kipindi
sasa.
Rage na
Kaburu, ingawa wamekuwa hawaonyeshi, lakini wamekuwa hawaelewani kutokana na
mitazamo ya kimaendeleo, hali iliyochangia Kaburu kuamua kuachia ngazi kwa
manufaa ya klabu hiyo.
Lakini leo
walikumbatiana, wakazungumza wakionyesha kubadilishana mawazo halafu kwa pamoja
wakapiga picha.
0 COMMENTS:
Post a Comment