March 31, 2014


Simba imeweka nyota wake watano sokoni ambao wanatarajiwa kumaliza mikataba yao msimu huu huku wakiwa na matumaini madogo ya kuongezewa mikataba.


Nyota hao ni pamoja na mlinda mlango Yaw Berko, Henry Joseph, Haruna Shamte, Ramadhani Chombo ‘Redondo’ na Uhuru Selemani.

Chanzo cha habari kutoka ndani ya timu hiyo kimesema mikataba ya nyota hao inamalizika mwishoni mwa msimu huu na Simba haina mpango wa kuwaongezea mikataba.

Chanzo kilisema kuwa, kwa sasa Simba ipo katika harakati za kusaka vipaji ndani na nje ya Tanzania ili kuweza kuhakikisha wanapata wachezaji wenye uwezo na kiwango cha juu zaidi.

“Hao (Berko, Henry, Shamte, Redondo na Uhuru), mikataba yao inamalizika ila uwezekano wa kuwapa mikataba mipya ni mdogo kwa sababu tunazingatia suala la uwezo na viwango vyao, japo tutaangalia na mahitaji ya mwalimu pia ili kuweza kujipanga vyema kwa ajili ya msimu ujao wa ligi kwa kusajili vijana wenye uwezo mzuri,” kilisema chanzo.

Simba imekuwa haina mwenendo mzuri msimu huu na ipo katika nafasi ya nne kwenye Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 36.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic