March 31, 2014


Timu ya Mbeya City ipo katika wakati mgumu kutokana na wachezaji tegemeo wa kikosi hicho kuwa majeruhi, wakiongozwa na mshambuliaji Mwagane Yeya anayeumwa mgongo.


Wachezaji wengine walio na majeraha ni winga Richard Peter ambaye amevunjika mbavu na beki John Kabanda mwenye maumivu ya bega.

Yeya na Kabanda walipata maumivu hayo katika mchezo dhidi ya JKT Ruvu wakati Peter aliumia kwenye mtanange dhidi ya Rhino Rangers.

Kocha Mkuu wa Mbeya City, Juma Mwambusi, alisema hajui wachezaji hao watarejea lini dimbani, lakini akakiri kwamba kuna hatari ya kuwakosa katika michezo yote iliyobaki.

“Nasikitika kuendelea kuwakosa wachezaji wangu ambao ni muhimu, wanakosa michezo hii ya mwisho kutokana na kuwa majeruhi.

“Lakini bado ripoti ya daktari haijatoka na kufahamu kuwa watarejea lini uwanjani, japo tumebakiza michezo michache. Kwa upande wa Richard Peter aliyevunjika mbavu, hataweza kucheza tena mechi zilizobaki hadi msimu ujao kutokana na hali yake,” alisema Mwambusi.


Nyota hao ni miongoni mwa wale waliofanya Mbeya City kuwa tishio msimu huu. Timu hiyo ipo katika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic