Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF) tunalaani vikali fujo na uhabirifu wa mali unaofanywa na washabiki
viwanjani wakati mechi mbalimbali zikiwemo zile za kimataifa na ligi za hapa
nchini.
Tunaiomba radhi Serikali kwa uharibifu
wa viti uliotokea kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Yanga ya
Tanzania na Al Ahly ya Misri iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Uharibifu huo wa viti umesababisha
hasara ya sh. milioni 15 kwa wamiliki wa uwanja huo ambao ni Serikali. TFF
tutalipa fedha hizo kwa Serikali kutokana na uharibifu huo.
Tunaendelea kuchunguza tukio hilo, huku
tukijiandaa kutoa adhabu kwa klabu na washabiki husika kulingana na kanuni
zetu. Adhabu itakuwa kali ili iwe fundisho kwa wengine.
Kwa mujibu wa Serikali, viti kumi
viling’olewa na kutupwa ovyo ovyo uwanjani wakati vingine 40 viliathirika
kutokana na vurugu za watazamaji hao.
Tumebeba dhamana ya kulipa uharibifu
huo kwa vile TFF ndiyo wenye dhamana ya kusimamia mechi za kimataifa, na ndiyo
tulioomba idhidi ya kutumia uwanja huo.
Kwa vile sasa baadhi ya washabiki,
wapenzi na wanachama wa klabu mbalimbali nchini wanataka kufanya suala la
uharibifu kuwa la kawaida na mazoea, Serikali inakusudia kuchukua mapato yote
ya mchezo husika endapo kutatokea uharibifu.
Pia kuruhusu uwanja kutumiwa bila
watazamaji kwa baadhi ya mechi, na kutoruhusu uwanja huo kutotumika kabisa kwa
baadhi ya mechi.
0 COMMENTS:
Post a Comment