March 10, 2014


Mshambuliaji wa Yanga, Emmanuel Okwi amesema huu ni wakati mwafaka kwa klabu yake kutazama mbele badala ya kuanza kuonyooshenea vidole.

Okwi amesema hakuna haja ya mtu kumyoonyesha kidole mwingine, badala yake ni kuangalia nini cha kufanya baada ya kupoteza mechi yao dhidi ya Al Ahly.

Mimi niwashukuru mashabiki wetu wanaotuunga mkono, wala hatuna sababu ya mmoja kumnyooshea kidole mwingine, badala yake tuangalie mbele yetu tuna majukumu yapi.
Si sahihi kuanza kunyoosheana vidole, si sahihi. Mpira una njia zake za kupita na matokeo yake moja ni kupoteza, lakini kila mmoja ameona walichokifanya Yanga, alisema Okwi.

Yanga imetolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kufungwa mikwaju ya penalti 4-3 na mabingwa wa Afrika Al Ahly. Ndani ya dakika 90 ilipoteza kwa bao 1-0 kama ilivyoshinda jijini Dar.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic