RAIS WA TFF, JAMAL MALINZI |
Wang’amuzi vipaji 28 wanakutana
Lushoto mkoani Tanga kwa siku saba katika mpango maalumu wa maboresho ya Taifa
Stars ambapo watatoka na orodha ya mwisho ya wachezaji waliopatikana katika
mechi za maboresho hayo zilizochezwa nchi nzima.
Katika kikao hicho, wang’amuzi hao
watapitia majina ya wachezaji walioteuliwa ikiwemo kuwaangalia tena kwenye
video kwa vile mechi zote zilirekodiwa. Wachezaji watakaoteuliwa katika mpango
huo baadaye wataingia kambini mkoani Mbeya.
Wang’amuzi vipaji ambao wanaoondoka
Machi 9 mwaka huu kwenda Lushoto ni Abdul Mingange, Boniface Pawasa, Charles
Mkwassa, Dan Korosso, Dk. Mshindo Msolla, Edward Hiza, Elly Mzozo, Hafidh
Badru, Hamimu Mawazo, John Simkoko, Jonas Tiboroha, Juma Mgunda na Juma
Mwambusi.
Kanali mstaafu Idd Kipingu, Kenny
Mwaisabula, Madaraka Bendera, Madaraka Selemani, Mbarouk Nyenga, Mohamed Ally,
Mussa Kissoky, Nicholas Mihayo, Peter Mhina, Salum Mayanga, Salvatory Edward,
Sebastian Nkoma, Sekilojo Chambua, Selemani Jabir na Shabani Ramadhan.
Wengine ni Mjumbe wa Kamati ya
Utendaji ya TFF ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi, Kidao Wilfred,
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya
Vijana, Ayoub Nyenzi, Kaimu Mkurugenzi wa Ufundi, Salum Madadi na Mshauri wa
Rais (Ufundi), Pelegrinius Rutayuga.
0 COMMENTS:
Post a Comment