March 10, 2014

BALOZI HAMZA AKIWA NA FAMILIA YAKE, HAPA ALIINGIA VYUMBANI KUWAPA POLE YANGA MARA BAADA YA KUPOTEZA MECHI DHIDI YA AL AHLY
Mabingwa wa Tanzania Bara, Yanga wamerejea jijini hapa kutoka Alexandria na moja kwa moja kupata mwaliko mzito kwa Balozi wa Tanzania nchini Misri.


Balozi Mohammed Haji Hamza  amewakaribisha Yanga ambao amewaandalia hafla fupi na atapatanafasi ya kujumuika pamoja nao na kubadilishana nao mawazo.

Balozi Hamza pamoja na maofisa wengine wa ubalozi wamekuwa bega kwa began a Yanga tokea imewasili jijini hapa na baadaye kwenda Alexandria kupambana na Al Ahly.

Katika mechi ya mjini Alexandria ambayo Yanga ilitolewa kwenye Ligi ya Mabingwa na wenyeji al Ahly kwa mikwaju ya penalty, Balozi Juma alikuwa kati ya waliofika uwanjani.


Baada ya hafla ya leo, kesho Yanga itakuwa katika maandalizi ya kurejea nchini na itatua jijini Dar es Salaam  Jumatano saa 12 asubuhi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic