April 5, 2014


Kocha Carlo Ancelotti amethibitisha kuwa atampumzisha mshambuliaji wake Cristiano Ronaldo katika mechi ya Jumamosi ya La Liga.

Kocha huyo amesema wameamua kufanya hivyo kwa ajili ya mechi ya pili ya Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya robo fainali dhidi ya Borussia Dortmund.
“Hana maumivu lakini anatakiwa kuwa vizuri zaidi na pia ni kuepuka kumkosa kabla ya mechi hiyo muhimu zaidi,” alisema.
Di María:"Amepona, lakini sina uhakika kama ataanza ingawa amekuwa akifanya mazoezi ye pekee na maalum.
Real Sociedad:"Ni timu ngumu, hawana aina moja ya uchezaji na ni kazi ngumu kuwathibiti, ila tutapambana.
Nafasi ya Cristiano:"Tunao watu, mfano Morata atacheza, ikishindikana yupo Isco na wengine.”
Bale vipi?"Nafikiri yuko safi kabisa, nafikiri bado hajawa na msimu mzuri lakini kila siku anabadilika na kuanza kuzoea."
Barça kuzuiwa na Fifa kusajili: “Kweli siwezi kulizungumzia, zaidi nazungumzia soka na si mambo hayo, si kazi yangu,” alisema Ancelotti.




0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic