Timu ya
Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) itacheza mechi ya kirafiki na Burundi (Intamba
Mu Rugamba) Aprili 26 mwaka huu ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya
muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro
Premium Lager tayari ipo kambini Tukuyu mkoani Mbeya ikijiandaa kwa ajili ya
mechi hiyo ikiwa na wachezaji waliopatikana katika programu maalumu ya kusaka
vipaji.
Baadaye wachezaji wengine wa Taifa
Stars ambao wapo nje ya programu ya kusaka vipaji wataungana na wenzao kabla ya
kutengeneza kikosi cha mwisho kitakachoivaa Burundi.
Mechi hiyo itakayofanyika Uwanja
wa Taifa, Dar es Salaam itachezeshwa na waamuzi wanaotambuliwa na Shirikisho la
Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kutoka nchini Kenya.
0 COMMENTS:
Post a Comment