April 5, 2014


Fahad Ally, Bukoba 
Simba imeeendelea na wimbi la sare au kufungwa baada ya kutoka sare ya mabao 1-1 dhidi ya Kagera Sugar.


Katika mechi hiyo ya Ligi Kuu Bara iliyochezwa kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini hapa, Simba ilianza kupata bao lake katika dakika ya 35 kupitia Zahoro Pazi lakini wenyeji Kagera wakasawazisha katika dakika ya 61.

Sare hiyo, inazidi kuididimiza Simba na inawezekana kabisa Simba ikaingia katika wakati mgumu hata kupata nafasi ya nne mwishoni mwa ligi hiyo.
Simba imecheza mechi hiyo bila ya mshambuliaji wake Amissi Tambwe raia wa Burundi na beki Mganda Joseph Owino ambao ni wagonjwa.

Katika mechi nyingine ya ligi hiyo, Mbeya City imelazimishwa sare ya bila kufungana na wenyeji wake Ashanti United kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar.

Mchezo ulikuwa na ushindani mkubwa na kosakosa nyingi lakini mwisho mechi hiyo ikamalizika bila ya bao hata moja

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic