Mabingwa wa soka Tanzania, Azam FC
wamefanikiwa kumsainisha kiungo Frank Domayo.
Domayo aliyekuwa akikipiga Yanga
amefanikiwa kusaini mkataba wa miaka miwili na mabingwa hao mjini Mbeya akiwa katika kambi ya timu ya taifa, Taifa Stars inayojiandaa kukipiga na Malawi.
Siku moja iliyopita, Azam FC ilimsajili
mshambuliaji nyota wa Yanga, Didier Kavumbagu raia wa Burundi.
Maana yake ndani ya wiki moja Azam FC
wamesaini wachezaji wawili wa Yanga.
0 COMMENTS:
Post a Comment