April 23, 2014


Kipa wa Chelsea, Petr Cech hataitumikia timu hiyo katika mechi yoyote msimu huu.

Cech amewekwa nje msimu wote hadi mwisho kutokana na majeraha aliyoyapata katika mechi ya kwanza ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Atletico Madrid.

Taarifa zimeeleza, kutokana na maumivu hayo baada ya kupatiwa matibabu kwenye hospitali moja mjini Madrid, kipa huyo atalazimika kuikosa Chelsea hadi mwisho wa msimu.

Lakini bahati mbaya tena kwa Chelsea, itamkosa nahodha wake John Terry ambaye aliumia katika mechi hiyo.

Imetangazwa, Terry hatacheza mechi ijayo dhidi ya Atletico Madrid jijini London.

Hivyo Chelsea, itakuwa na nafasi ya kumtumia tena, iwapo tu itavuka na kuingia fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa kuwa anatarajiwa kuwa fiti.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic