April 5, 2014

MUUAJI WA KWANZA WA BAYERN MUNICH

Hatimaye rekodi ya Bayern Munich kucheza Bundesliga bila ya kufungwa msimu huu imeharibika baada ya kuchapwa bao 1-0 na vibonde.

Bao lililofungwa na Sascha Moelders wa  Augsburg katika dakika ya 31 ambao ni vibonde wa ligi hiyo, imeharibu rekodi hiyo ya kucheza mechi 53 bila ya kufungwa hata moja.


Bayern Munich inayonolewa na Pep Guardiola wanatarajia kucheza na Manchester United katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, wiki ijayo.


MEchi ya kwanza mjini Manchester timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1 na kuanza kuvunjwa kwa rekodi ya kutofungwa kunaonyesha kuwashtua mashabiki wake.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic