April 29, 2014


Mshambuliaji Didier Kavumbagu ametua na kujiunga na mabingwa wa Tanzania Bara, Azam FC.

Kavumbagu amesaini kuichezea Azam FC kwa misimu miwili, hali ambayo inaonyesha kutakuwa na ushindani mkubwa katika nafasi ya ushambuliaji.
Azam FC ina John Bocco ambaye ndiye nahodha pamoja na Gaudance Mwaikimba.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Kavumbagu alisema anaanza kwa kuwashukuru Yanga kwa ujumla kutokana na kumuunga mkono muda.
“Lakini pia upande wa Azam FC ambao wameniona, sasa mimi ni mchezaji wa Azam FC,” alisema Kavumbagu raia wa Burundi.

Kavumbagu alikuwa tegemeo la Yanga katika upachikaji na utengenezaji mabao.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic