April 29, 2014


Kocha wa Simba, Zdravko Logarusic amesema maisha saaafi kwao Croatia na sasa anajipanga upya.

Logarusic ambaye amerejea kwao baada ya msimu kwisha amesema anaendelea na maisha vizuri huku akiendelea kutafakari.
“Hapa kila kitu kinaenda vizuri, nimekuta kila kitu safi na sasa naendelea na mapumziko.
“Lakini natafakari mambo kadhaa kuhusiana na kuanza msimu mpya ingawa sina uhakika itakuwa Simba au kwingine. Kila siku mambo yanabadilika na ndiyo maana ya maisha,” alisema.
Logarusic amefanya mazungumzo na Zacharia Hanspope ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba ambaye amemuambia asikilizie kwanza.

Kinachoonekana Hanspope anataka kuangalia upepo wa uchaguzi ili kujua nini kitafanyika baada ya hapo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic