April 7, 2014





Kocha wa Yanga, Hans van Pluijm, amesema kuwa amesema wachezaji wake, Juma Kaseja na Emmanuel wana matatizo binafsi ndiyo maana akaamua kutowatumia kwenye mechi dhidi ya JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar, jana.


Kocha huyo raia wa Uholanzi amesema kuwa Kaseja na Okwi hawakuwemo kwenye kikosi chake kwa sababu hakuwa nao hata mazoezini, hivyo hawezi kumtumia mchezaji ambaye hajafanya naye mazoezi na kusisitiza kuwa wawili hao wana matatizo yao binafsi kama inavyoripotiwa.

“Sikuwa nao kwenye mazoezi, ndiyo maana sijawatumia, wana matatizo yao binafsi kama ambavyo inaandikwa kwenye magazeti, siwezi kulizungumzia zaidi hilo, lakini ifahamike hivyo,” alisema kocha huyo bila kuwa tayari kufafanua matatizo yapi.

Okwi amekuwa nje ya kikosi hicho kwa siku kadhaa sasa ikiripotiwa kuwa ana madai yake ya fedha ambayo hajakamilishiwa mpaka sasa wakati wa usajili, huku taarifa za ziada zikisema kiasi ambacho anadai ni shilingi milioni 60, wakati Kaseja haijajulikana matatizo yake.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic