April 26, 2014


Taifa Stars leo inaivaa Burundi katika mechi ya kirafiki kusherekea sikukuu ya Muungano.
Mechi hiyo itapigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam huku wachezaji kadhaa wakisubiriwa kwa hamu.

Mfano ni Amissi Tambwe ambaye ni mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara ambaye atakuwa katika kikosi hicho.

Lakini tegemeo kubwa la Burundi ni mshambuliaji Amisi Cedrick anayekipiga katika timu ya Rayon Sports ya Rwanda, anavaa jezi namba 17 kama hatabadili leo, namba ambayo tambwe huvaa pia.
Msimu uliopita aliibuka na mabao 16 na kuonyesha yeye si mchezo, lakini msimu huu anaongoza kwa ufungaji ligi ikiwa imebaki mechi mbili. Tayari ameishatupia mabao 13.
Cedrick mbaya kweli, pamoja na kuwa mfungaji bora wa Rwanda, lakini ana uwezo mkubwa wa kutoa pasi za mabao. Hivyo atakapocheza na Tambwe, mabeki wa Stars wamtupie jicho kweli!

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic